Sikiliza Ujumbe hapa⤵
Migogoro ya silaha inaharibu sana maisha ya raia, hasa wanawake, watoto na wazee. Watu wengi wanakosa chakula, matibabu na usalama.
Wimbo wa Geneva Call inatoa ujumbe muhimu ya kulinda raia, kuheshimu maisha ya binadamu na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia watu wenye mahitaji.
Wakati wa vita, pande zote zinazohusika zinapaswa kuheshimu sheria za kibinadamu, kulinda raia na kuruhusu watu kupata chakula, maji na matibabu.
Kila mmoja ana jukumu la kujenga amani kwa kukataa chuki, kuhimiza mazungumzo na kusaidia watu walio katika mazingira magumu.
Kulinda raia ni kulinda maisha. Kusaidia wahitaji ni kuleta matumaini. Amani ni jukumu letu sote !
