Baada ya kuthibitishwa kwa visa viwili vya Ugonjwa wa Virusi vya Ebola katika Eneo ya Afya wa Mambasa, ikiwemo kifo cha mgonjwa mmoja, msimamizi wa wilaya ya Mambasa, Kamisha Mkuu Matadi Muyampandi Jean-Baptiste, ametoa wito kwa wanainchi kuzingatia kikamilifu hatua za kujikinga zidi ya ugonjwa huo. Kutokana na Mambasa kuwa eneo jipya lililoathiriwa na mlipuko wa Ebola katika mkoa wa Ituri, mamlaka za afya zinahimiza umakini wa jamii na ushirikiano na timu za afya ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
Tumusikilize mnyapara wa mtaa wa Mambasa :

